33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wahamiaji haramu 18 wakamatwa Kilimanjaro

Na Upendo Mosha,Mwanga

Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro limewakamata wahamiaji haramu 18 Raia wa Ethiopia kutokana na kosa la kuingia nchini bila kibali jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari wilayani Mwanga jana, Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Amon Kakwele amesema wahamiaji hao walikamatwa Mei 06, mwaka huu katika Kata Kileo Mwanga.

Amesema wahamiaji hao walikamatwa wakati Askari wa jeshi hilo wakiwa katika doria katika eneo hilo ambapo waliwakuta wakiwa barabarani wakirandaranda.

“Askari waliokuwa doria katika eneo la Kileo hapa Mwanga walikamatwa wahabeshi 18 wakiwa njiani wakirandaranda kutafuta usafiri kwa sasa wapo kituo cha polisi Mwanga,”amesema Kamanda Kakwele.

Katika hatua nyingine Jeshi hilo limewakamata watu wawili kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya aina ya bangi na mirungi.

“Tumewakamata watu wawili kwa kusafirisha dawa za kukevya aina ya bangi misokoto 3,946 sawa na kilo 14 pamoja na mirungi kilo 39,”alisema Kakwele.

Kamanda Kakwele amewataja watu hao kuwa ni Mchao Togolani (32) Mkazi wa Same ambaye alikamatwa maeneo ya Bomang’ombe wilayani Hai na Fatuma Elias (45) Mkazi wa Mererani aliyekamatwa wilayani Mwanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles