25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wagonjwa wa afya ya akili waongezeka Muhimbili

AVELINE KITOMARY

DAR ES SALAAM
IKIWA kesho ni siku ya ugonjwa wa akili Duniani takwimu za Hospitali ya Taifa ya Muhimbili zimeonesha ongezeko la idadi ya wagonjwa wa afya ya akili hadi asilimia 10.8.

Takwimu hizo zinaonesha kuwa kwa mwaka 2018/2019 idadi ya wagonjwa ilikuwa ni 29,166 huku mwaka 2019/2020 idadi ikipanda na kufikia 32,307.

Akizungumza na Waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Idara ya Afya ya Akili Muhimbili -Mloganzila Dk Fileuka Ngakongwa alisema sababu za kuongezeka kwa ugonjwa huo ni Sonona (Depression disorder) kwa asilimia 15 hadi 38.

“Pia idadi ya ongezeko la wagonjwa hospitalini inachangiwa na upatikanaji wa huduma hii na uelewa wa jamii kuongezeka hivyo mtu anapoumwa anapelekwa hospitali.

“Hospitali inahudumia wagonjwa wa ndani na nje ambapo kwa mwaka 2018/2019 wagonjwa wa nje walikuwa 20,571 na mwaka 2019/2020 wagonjwa wa nje walikuwa 21,183,”amesema.

Kwa upande wa huduma amesema zimeendelea kuboreshwa ambapo idadi ya watoa huduma na vifaa vya kisasa vimeongezwa pia.

“Katika kipindi cha miaka mitano Kuna madaktari bingwa 12 pamoja na hayo idara inaendelea kutoa na kusimamia mafunzo ya ziada ya afya ya akili,saikolojia na tiba,”ameeleza.

Amesema kuwa upatikanaji wa dawa umefanya wagonjwa wengi kupona na kurudi katika hali zao za kawaida.

“Tunatoa huduma kwa waraibu wa dawa za kulevya kwa kushirikiana na wizara ya Afya na pia kuna kliniki ya vijana na watoto imesaidia katika matibabu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles