26.1 C
Dar es Salaam
Friday, December 9, 2022

Contact us: [email protected]

Muhongo Ahaidiwa kura za kishindo Musoma vijijini

SHOMARI BINDA, MUSOMA

Wananchi wa vijiji vya Kata ya Mugango na Tegeruka vilivyopo jimbo la Musoma vijijini wameahidi kumchagua tena Profesa Sospeter Muhongo kwa kumpa kura za kishindo katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28, mwaka huu.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye mikutano ya kampeni kwenye vijiji vya Kwibara, Mayani na Kataryo, wananchi hao walisema bado wanayo imani na mgombea huyo anayepeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

walisema kwenye vijiji vyao kwa miaka mingi wamekuwa wwkisumbuliwa na adha ya kukosa umeme lakini kupitia mgombea huyo hivi sasa umeme unawafikia na kwamba amewasaidia pia kuwaondolea changamoto nyingine nyingi.

Licha ya umeme wananchi hao walisema Muhongo amehamasisha suala la elimu kwa kuchangia ujenzi wa shule mpya kwenye vijiji vyao na kudai wapo tayari kumchagua tena ili awapekee maendeleo zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,734FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles