‘Tymilyfe’ aiweka wazi LOCO

0
214

CHRISTOPHER MSEKENA


KUTOKA jijini London, Uingereza msanii anayefanya poa pande hizo, Samson Otieno ‘Tymilyfe, amerudi kivingine na wimbo, LOCO.


Akizungumza na MTANZANIA, Tymilyfe alisema baada ya mapumziko yaliyosababishwa na ugonjwa wa corona, amewaletea burudani mashabiki kupitia ngoma hiyo ya mapenzi.


“Watu wengi sasa hivi wanataka burudani, nikaona niwape LOCO, huu ni wimbo ambao ninamsifia msichana wa Kiafrika, naonyesha jinsi warembo wa Kiafrika walivyobarikiwa na Mungu pia video tayari imetoka ipo kwenye chaneli yangu ya YouTube ya Tymilyfe,” alisema msanii huyo mwenye asili ya Kenya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here