Na Mwandishi wetu
Wadau mbalimbali wa teknolojia wameshauri ubunifu wa hali ya juu katika sekta ya elimu ili kuongeza kasi ya maendeleo nchini kupitia Tehama.
Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha uvumbuzi cha Dar Teknohama Business Incubator (DTBI) Dk George Mulamula, aliyekuwa akizungumza katika mkutano uliohusu mustakabali wa elimu katika Wiki ya Ubunifu leo (Machi 29, 2019), amesema elimu ni muhimu kwa kuwa ndio msingi wa kila kitu nchini.
Amesema ni jukumu la walimu na wanataaluma kuvumbua mbinu mpya za kusaidia kufundishia wanafunzi mbali na zile zilizozoeleka.
“Uvumbuaji wa mbinu tofauti za ufundishaji kama matumizi ya ‘animations’ ni muhimu kwa kuwa yanampa mwanafunzi wigo mpana wa kufikiri na kuelewa tofauti na mbinu nyingine tulizozizoea,” amesema.
Mshauri wa masuala ya elimu kutoka Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (DFID), Arianna Zanolini amesema walimu wanajukumu la kujua ni kwa namna gani wanaweza kubadili sekta hii kuwa bora zaidi.