30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Vitambulisho vya machinga vyayeyusha mapato

Na Amina Omari

-TANGA

VITAMBULISHO vya wajasiriamali vilivyotolewa na Rais John Magufuli vimesababisha Halmashauri ya Jiji la Tanga kukosa mapato huku vyanzo vyake vya mapato 15 kufutika na hivyo kushindwa kutekeleza miradi ya maendeleo.

Hayo yamesemwa jana na Meya wa Jiji la Tanga, Seleboss Mustafa wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani cha kuwasilisha taarifa ya utendaji kazi kwa kila kata.

Alisema kuwa jiji hilo lilikuwa na jumla ya vyanzo vya mapato 38 ambavyo vilikuwa vinatarajiwa kuliingiza halmashauri hiyo bajeti ya Sh bilioni 15 lakini ugawaji wa vitambulisho kwa wafanyabiashara wasio stahiki imesababisha kasoro hiyo.

Alisema kuwa zoezi hilo kwa kiasi kikubwa limekwamishwa na watendaji wa kata na mitaa kwa kushindwa kusimamia kwa ukaribu ugawaji wa vitambulisho hivyo kwa watu wasiostahili.

“Kwa hili watendaji  mmechangia kutukwamisha kwani mpaka sasa mapato yetu yamefikia asilimia 65 huku ikiwa bado mwezi mmoja tuu mwaka wa serikali uishe, lakini nyie mmetoa vitambulisho kwa watu ambao hawakustahiki,” alisema.

Alisema ukosefu huo wa mapato umesababisha halimashauri hiyo kushindwa kutekeleza shughuli za kijamii kama usafi wa masoko pamoja na marekebisho ya taa za barabarani.

“Watendaji wameshindwa kutafsiri nia ya Rais kwani vitambulisho vimetolewa hadi kwa wavuvi pamoja na wafanyabiashara wakubwa wenye maduka sasa wote wamegeuka na kuwa wajasiriamali,”alisema Mustafa.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Tanga, Ramadhani Possi,  alisema kuwa ufinyu wa bajeti umesababisha miradi mingi ambayo walikuwa wamepanga kuitekeleza kushindwa kutekelezwa kwa wakati .

“Kwa sasa tunajipanga kuboresha miundombinu ya shule zetu kwa kujenga madarasa mapya ukarabati ya vyoo pamoja na madawati ambapo tunafanya kila pale tunapopata fedha japo kidogo,”alisema Possi.

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Selemani Zumo aliwataka watendaji wa jiji kuhakikisha wanafanyakazi kwa uwadilifu na kujituma pamoja na kujua mipaka ya kazi zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles