30.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

‘Migogoro ya ndoa yazidi kuongezeka’

Na Mwandishi Wetu

-Dodoma

KWA kipindi cha miezi tisa kuanzia Julai 2018 hadi Machi mwaka huu jumla ya mashauri ya ndoa 16,832 yalipokelewa ikilinganishwa na mashauri 13,382 ya mwaka 2017/18 hali ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 34 ya migogoro ya ndoa nchini.

Akizungumza jana mjini hapa kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii , Dk. John Jingu,  Mkurugenzi wa Watoto wa Wizara hiyo Mwajuma Magwiza,  aliitaja changamoto ya maadili ya mmomonyoko wa maadili kuwa chanzo cha migogoro ya ndoa hapa nchini.

Magwiza alisema vitendo vya ukatili kwa watoto ndani ya familia vimekithiri huku wahausika wakubwa wa vitendo hivyo wakiwa  wanafamilia hili likijionesha katika takwimu za Jeshi la Polisi za mwaka 2017 zinaonesha kuwa jumla ya matukio ya ukatili kwa watoto 13,457 yameripotiwa na Jeshi la Polisi.

Alivitaja vitendo hivyo kuhusisha ukatili wa kingono wenye matukio 3,583, mimba za utotoni 1,323 akiongeza kuwa taarifa jeshi hilo imeonesha matukio ya mikoa ya kipolisi yenye ukatili mkubwa kuwa ni Kinondoni matukio 2,426, Dodoma 1,283, Tanga 164, Tameke 984 na Arusha Matukio 972.

Wakati huo huo Serikali imewataka  baadhi ya wazazi nchini kuacha tabia ya kutoa kipaumbele cha elimu kwa watoto wa kike kama ilivyo kwa watoto wa kiume jambo ambalo linakwamisha juhudi za Serikali katika kuhakikisha usawa wa kijinsia unatekelezwa katika nyanja zote bila ubaguzi wa kijinsia.

Akisoma hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Dodoma, Mhandisi Happiness Mgalula ambaye pia ni Katibu Tawala Masaidizi Mkoa wa Dodoma aliongeza kuwa ni lazima elimu itolewe kwa kuzingatia usawa wa kijinsia.

Mgalula aliwataka wazazi na walezi kutoa kipaumbele cha elimu kwa watoto wote bila kujali jinsia ikiwa ni hatua muhimu  ya kutekeleza ahadi ya Rais kwa vitendo ya utoaji elimu bure kwa wanafunzi nchini.

Alisema Tanzania bado inakabiliwa na tatizo la mila potofu akizitaja mila hizo kuwa ni kuwa ni mimba na ndoa za utotoni, haki ya wanawake kumiliki ardhi, vipigo kwa wanawake akiutaja Mkoa wa Dodoma kuwa wa pili kitaifa katika vitendo vya ukatili.

Hata hivyo aliwataka wanafamilia kuhakikisha wanakuwa ana afya bora kwa kuhakikisha wanakuwa na vitambulisho vya bima ya afya, elimu na akina mama wajawazito kuhakikisha wanaenda hospitali ili kupata huduma ya afya kwa mama na mtoto.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles