ADDIS ABABA, ETHIOPIA
MARAIS wa nchi za Umoja wa Afrika (AU) waliokutana hapa juzi kwa kikao cha siku mbili wamejadili kuhusu ufadhili wa miradi ya maendeleo ya umoja huo, tatizo la uhamiaji na ufumbuzi wa migogoro katika nchi kadhaa.
Mwenyeketi mpya wa Umoja huo, Rais Paul Kagame wa Rwanda amesema bila ya kuwepo mshikamano maendeleo ni ndoto barani Afrika.
Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Rais Alpha Conde wa Guinea, amesema kuwa matatizo ya Afrika lazima yatatuliwe na Waafrika wenyewe.
Conde amekosoa vikali uwajibikaji wa vikosi vya Umoja wa Mataifa barani Afrika na kupendekeza kuweko vikosi vya kikanda vya Waafrika wenyewe chini ya Umoja huo.