33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Vijana wamlazimisha Rais Nigeria kubadili msimamo

Lagos, Nigeria

Maandamano yaliotanda kote nchini Nigeria kwa sababu ya kikosi maalum cha polisi cha kukabiliana na wizi wa mabavu (Sars) ni ishara kwamba vijana wanapaza sauti yao wakidai mabadiliko katika nchi hiyo maarufu barani Afrika ambayo imekumbwa na sifa ya utawala mbaya tangu ilipopata uhuru wake miaka 60 iliyopita.

Licha ya kumlazimisha rais kuvunja kikosi hicho cha polisi, bado wanadai mabadiliko kamili katika kikosi kizima cha polisi na maafisa waliotekeleza dhulma wakabiliwe na mkono wa sheria.

Lakini ni zaidi ya madai hayo kwa sababu wimbi hilo la maandamano limetoa fursa kwa vijana wengine kote nchi humo kuonesha kutoridhika kwao na serikali.

Mitaani, wanaoandamana ni vijana ambao wengine wametia nywele rangi, wako waliotoboa masikio na hata kuchora tattoo mwilini.

Ni kundi ambalo ni rahisi sana kwa maafisa wa usalama kulipachika jina la wahalifu, lakini ukweli ni kuwa hawa ni vijana wanaofanyakazi kwa bidii ambao hawategemei serikali.

Wengi wao wana umri wa kati ya miaka 18 na 24 na katika maisha yao hawajawahi kuwa na umeme thabiti, hawakupata elimu ya bure nchini mwao huku masomo yao chuo kikuu yakirefushwa kwasababu ya wahadhiri kushiriki maandamano ya mara kwa mara.

Matatizo wanayopitia mikononi mwa polisi kunaakisi yale ambayo vijana wa taifa hilo wanayapitia kwa ujumla.

“Ni kipi ambacho nimenufaika nacho tangu nimezaliwa katika nchi hii ?” Victoria Pang, 22, aliyehitimu ameuliza, aliyeshiriki moja ya maandamano katika mji mkuu wa Abuja na mmoja kati ya wanawake ambao wamekuwa mstari wa mbele katika maandamano.

“Wazazi wetu wanasema kuna wakati mambo yalikuwa mazuri lakini sisi hatujawahi kushuhudia hilo,” alisema.

Maofisa wa polisi nchini Nigeria kwa ujumla wana sifa ya ufisadi, kutenda unyama na kutojali haki za binadamu lakini watu hapa wanahisia kali dhidi ya kundi la Sars ambalo limekuwa na tabia ya kutesa vijana.

Vijana wanaosemekana kujiweza kifedha, yaani wenye gari nzuri, kipakatalishi au waliochora ‘tattoo’ au kufuga ‘dreads’ hufuatwa sana na maafisa wa kikosi cha Sars.

“Kuna wakati watu wa mahali ninapoishi waliita mafisa wa polisi kunikamata kwasababu tu kila wakati nilikuwa nyumbani na ninaishi maisha mazuri,” Bright Echefu, 22, mtaalamu wa utengenezaji tovuti aliyeungana na waandamanaji amesema katika mazungumzo na BBC huko Abuja.

Kwa kipindi kirefu michoro ya tattoo, nywele za dreadlocks, kutoboa masikio na mitindo ya maisha inayosemekana kinyume na maadili kumechukiliwa kama kushindwa kujukumika kwa familia, mashirika ya kidini, jamii na hata shule. Serikali ya Sudan yaonywa kuhusu machafuko yatakayotokea ikianzisha uhusiano wa kawaida na Israel

BBC

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles