26.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Uzinduzi Safari ya Beach waisimamisha Mabibo

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Mamia ya wakazi wa Mabibo na Manzese wamejitokeza kushudia uzinduzi wa pambano kubwa la ngumi za kulipwa lililopewa jina la ‘Safari ya Beach’ uliofanyika Septemba 15,2023 kwenye viwanja vya Mpakani, jijini Dar es Salaam.

Katika uzinduzi huo kulikuwa na burudani mbalimbali za muziki pamoja na utambulisho wa baadhi ya mabondia wanakaopanda ulingoni siku hiyo ambao walipata nafasi ya kila mmoja kumtambia mpinzani wake.

Mabondia mbalimbali kutoka Manispaa zote za Dar es Salaam na nje ya nchi, wanatarajiwa kuoneshana ubabe Oktoba 28, 2023 katika fukwe za Msasani.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Promota wa pambano hilo Meja Selamani Semunyu kutoka Peaktime Media, amesema zaidi ya mabondia 50 watapanda ulingoni siku hiyo wakiwamo chipukizi na wakongwe.

Meja Semunyu amesema lengo lao ni kuhakikisha wanaibua vipaji kutoka mtaani ili kupata mabondia wazuri watakaotangaza Tanzania.

“Kazi kubwa tunayofanya ni kuinua vipaji, tunaomba tuwape sapoti hawa vijana sababu tunatengeneza mabondia wapya ambao baadaye watapeperusha bendera ya Tanzania baada ya hawa waliopo watu wazima ambao muda wao ni mchache wa kucheza ngumi.

“Mabondia hawa wana mashabiki wengi sana, umeona hapa hakuna bondia mkubwa alikuja lakini watu wamejaa. Ninaomba wadhamini na wadau wengine wajitokeze tusapoti hivi vipaji,”amesema Meja Semunyu.

Baadhi ya mabondi watakaochapana siku hiyo ni Said Tores maalufu Kichwa Kisicho na Ubongo dhidi ya Abdulrazack Hamisi ‘Bondia Mtoto’, Tasha Mjuaji na Ismail Boyka, Hassan Ndonga akizichapa na Oscar Richard.

Wengine ni Ramadhani Chicho dhidi ya Tampela Maurus, Martin Shekivuli na Gael Morris, huku pambano la uzito wa juu likimkutanisha William Chedi na Joseph Mboe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles