33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Ushirikina, ulevi watajwa vifo machimbo ya Moramu

Na ELIYA MBONEA

-ARUSHA

USHIRIKINA na ulevi unaochangia watu kutokuwa makini kwenye mgodi wa Moramu uliouwa watu watatu na kujeruhi wanne, unadaiwa kuwa chanzo cha mauaji yaliyotokea kwa miaka tofauti nyakati za Pasaka.

Mwaka 2013 siku ya Jumatatu ya Pasaka machimbo hayo yaliuawa watu 13, na Aprili 23, mwaka huu ajali hiyo imetokea tena ikiwa ni   Jumanne, siku moja baada ya Jumatatu ya Pasaka. 

Baadhi ya mashuhuda na wakazi wa eneo hilo waliliambia MTANZANIA jana kwamba zipo sababu mbalimbali zinazoweza kuchangia machimbo hayo kuendelea kuua watu vikiwamo ushirikina na ulevi.

Mkazi wa Sekei Moivaro tangu mwaka 1976, Zelothe Mollel alisema  wameshangaa kuona tukio la ajali kwenye machimbo hayo likitokea Sikukuu ya Pasaka. 

“Ajali ya mwaka 2013 ilitokea siku ya Pasaka ya Pili (Jumatatu ya Pasaka) na ajali ya juzi tena imetokea Jumanne siku moja baada ya Jumatatu ya Pasaka.

“Tukio hili lingetokea Jumatatu ya Pasaka ila tu kwa sababu kuliwekwa sheria hapa kwamba siku za mapumziko mgodi huwa unafungwa hakuna kufanya kazi,

“Jumatatu ya Pasaka hawakuingia, Serikali haiamini nguvu za giza lakini wananchi tunaamini kuna nguvu za giza ziko hapa. Kwa nini kila Pasaka damu za watu zinamwagika hapa?   

 “Hawa waliofunikwa walishindwa kukimbia manake unaweza kukuta mtu kalewa jana yake hivyo kukimbia haraka akawa ameshindwa,” alisema Mollel.

  Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Fabian Daqarro akizungumzia mazingira na usalama wa eneo hilo, alisema umewekwa ulinzi mkali kwenye machimbo hayo  kuzuia watu wasiendelee kuchimba. 

“Miili ya marehemu watatu ilipelekwa Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru kwa taratibu nyingine ambako gari liliharibika kabisa,” alisema DC Daqarro na kuongeza:

“Kikao cha Kamati ya Usalama ya wilaya cha dharura kitakaa na kujadili juu ya mchimbo yaliyopo wilayani kwetu ambako wataalamu wa madini watashiriki kujadili kwa kina na kuona nini kifanyike”.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles