Mwandishi Wetu, Dodoma
Ukubwa wa kitabu cha bajeti cha Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji umezua gumzo bungeni huku Waziri wa wizara hiyo Charles Mwijage akishindwa kusoma kitabu chote.
Kitabu hicho chenye kurasa 353 kilizua gumzo baada ya Waziri Mwijage kukiinua juu wakati akisimama kwa ajili ya kusoma Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa mwaka wa fedha 2018/19, ambapo wabunge walianza kucheka na kushangilia wakishangaa ukubwa wa kitabu hicho.
Wakati wabunge wakiendelea kucheka Spika wa Bunge, Job Ndugai alichombeza kwa kusema “Wabunge mnaona book (kitabu) hilo.”
Hata hivyo, Waziri Mwijage alisoma kitabu hicho lakini ilifika mahali akaagiza hotuba hiyo iingizwe kwenye kumbukumbu za bunge.