33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

UJUMBE WA AMANI WATAWALA SHEREHE ZA EID EL -HAJJ

SWALA: Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi (watatu kushoto) akiongoza waumini wa dini ya kiislamu kati swala ya Eid el Hajj iliyoswaliwa Uwanja wa Msikate tamaa Vingunguti, Dar es Salaam jana.

 

Na Waandishi Wetu, DAR/mikoani                     |                           


VIONGOZI wa Serikali na dini, wamehimiza waislamu  kudumisha amani, upendo na mshikamano katika jamii kama njia bora ya kusherehekea sikukuu ya Eid El-Hajj.

Walisema hayo jana, wakati wa swala ya Eid El-Hajj ambayo kitaifa ilifanyika katika uwanja wa Msife Moyo Vingunguti, Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa Baraza la Eid, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dk. Hussein Mwinyi, aliwataka waislamu kote nchini kudumisha amani na kuacha vitendo viovu vinavyoweza kusababisha kutoweka  tunu hiyo.

Alisema amani ndiyo tunu kubwa zaidi ambayo Tanzania imejaliwa na iwapo itatoweka hakutakuwa hata na nafasi ya kufanya ibada.

“Kama mlivyosema, hii ndiyo tunu kubwa zaidi, bila kuwapo hakutakuwa na nafasi ya kufanya ibada, kwa hiyo tuache vitendo vya uvunjifu wa amani ambavyo matokeo yake huwaathiri zaidi wanawake na watoto,” alisema Dk. Mwinyi.

Alilitaka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), kuhakikisha linafanya mambo yatakayoleta tija kwa waislamu wote na taifa kwa ujumla, badala ya kuwanufaisha watu wachache.

“Niwapongeze kwa juhudi mbalimbali ambazo mmezifanya katika kutoa wa huduma kwa jamii ikiwamo elimu.

“Niwasisitize mliombee taifa letu ambalo linapitia changamoto nyingi pamoja na Rais wetu, Dk. John Magufuli,” alisema Dk. Mwinyi.

Kaimu Katibu Mkuu wa Bakwata, Nuhu Jabir, alisema wakati wa kusherehekea sikukuu hiyo, ni vema waislamu wakaitumia kutafakari na kuthamini amani iliyopo nchini.

 Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles