Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Ujenzi wa Transfoma yenye uwezo wa Megawati 240 katika kituo kikuu cha kupoza na kusambaza umeme cha Ubungo, jijini Dar es Salaam, unatarajiwa kukamilika Mei mwaka huu.
Akielezea Maendeleo ya ujenzi wa transfoma hiyo, Mkuu wa Kituo cha Kupoza na Kusambaza umeme Ubungo, Mhandisi Joseph Msumali, amesema hatua inyofuata ni kujengea vifaa visaidizi ikiwamo kujenga msingi kwa ajili ya swichi zake kwa upande wa kilovoti 220 na kilovoti 132 na kufunga nyaya kwa ajili ya kuunganisha pande zote.
“Kukamilika transfoma hiyo kutaongeza nguvu katika Kituo cha umeme Ubungo kutoka MVA 300 hadi MVA 600 ambapo ni sawa na Megawati 480 na hivyo kutaongeza nguvu ya upatikanaji umeme wa uhakika katika Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani,” amesema.