28.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, January 19, 2022

Moto waua watu 70 Bangladesh

DHAKA, BANGLADESHD

MOTO mkubwa umelipuka katika vitongoji duni vya zamani vya makazi katika mji mkuu wa Bangladesh, Dhaka na kuua watu wasiopungua 70.

Mamlaka ya Zimamoto ilisema moto huo umeanzia katika ghala ambalo kemikali za kutengeneza bidhaa kadhaa za nyumbani zimekuwa zikihifadhiwa kinyume cha sheria, na baadaye ukaenea katika majengo mengine kwa kasi kubwa.

Miongoni mwa waliokufa ni watu waliokuwa katika sherehe ya harusi na wengine waliokuwa kwenye mgahawa.

Shughuli za uokozi zimetatizwa vikali na msongamano wa magari katika mitaa membamba ya kitongoji hicho.

Kamanda wa kikosi cha wazimamoto nchini Bangladesh, Ali Ahmed alisema bado wanaendelea kutafuta waathirika wa moto huo, na kwamba idadi ya waliokufa inaweza kuongezeka.

Moto huo ulianzia katika Mtaa wa Chawkbazar majira ya saa nne usiku kwa saa za Bangladesh.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
175,312FollowersFollow
531,000SubscribersSubscribe

Latest Articles