24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Uhamiaji yaeleza sababu ya kuwakamata waandishi wa CPJ

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam



Idara ya Uhamiaji nchini, imekiri kuwashikilia waandishi wa Kamati Maalumu ya Kuwalinda Wanahabari Duniani (CPJ), kwa kuingia nchini na kufanya shughuli kinyume na kibali cha matembezi walichokuwa nacho.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Idara hiyo, Ally Mtanda, waandishi hao Angela Quintal ambaye ni raia wa Afrika Kusini na Mumo Muthoki, raia wa Kenya walikuwa na kibali cha matembezi (holiday visit) cha miezi mitatu ambacho kinaisha muda wake Januari Mosi, mwaka 2019.

“Baada ya mahojiano, walikiri wameingia nchini kwa lengo la kufanya vikao na waandishi wa habari nchini wakati vibali vyao ni kwa ajili ya matembezi kinyume na Sheria ya Uhamiaji Sura ya 54, na kanuni zake za viza za mwaka 2016,” imesema taarifa hiyo.

Hata hivyo, baada ya uchunguzi idara hiyo imewaachia huru na kuwarejeshea hati zao za kusafiria kwa masharti ya kutoendelea na vikao hivyo kwa kutumia vibali vya matembezi walivyopewa.

Waandishi hao wanadaiwa kukamatwa katika Hoteli ya Southern Sun jijini Dar es Salaam na kushikiliwa hati zao za kusafiria na kisha kuachiwa huru.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles