24.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 24, 2023

Contact us: [email protected]

First Class kuzindua albam mpya

      Elizabeth Joachim Dar es salaam 

Bendi ya First Class Modern Taarabu inatarajia kuzindua albamu  mpya ya ‘Mama wa Hiyali’ Jumamosi Novemba 10 Hoteli ya Travetine Magomeni jijini Dar Es Salaam.

Mkurugenzi  wa Bendi  hiyo, Aboubakar Soud (Amigo) amesema albamu hiyo imebeba nyimbo sita huku wimbo mmoja wakimshirikisha msanii nguli wa nyimbo za taarabu, Khadija Kopa.

Amigo  amesema katika uzinduzi huo utahudhuliwa na Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto na wasanii ws taarabu, Khajida Kopa, Hawa Sabaha Salum na Patricia Hillary ambao pia watatumbuiza katika uzinduzi huo.

“Nimekuja kurejesha heshima ya muziki wa taarabu baada ya Mzee Yusuph kustaafu kwenye uzinduzi huu kutakuwa na vionjo vingi,” amesema Amigo

Naye Mkurugenzi wa Mipango wa bendi  hiyo, Said Safi amesema kundi hilo lenye wasanii 10 lilianzishwa Februari 14 Mwaka huu na limeanzishwa baada ya kuona muziki wa taarabu ukipoteza washabiki baada ya Mzee Yusuph kuacha kujihusisha na muziki.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,074FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles