22.3 C
Dar es Salaam
Saturday, July 13, 2024

Contact us: [email protected]

Uefa 16 borakuendelea leo

trophyMANCHESTER, ENGLAND

MICHUANO ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya inatarajia kuendelea leo kwa baadhi ya michezo kwa kuzitafuta timu ambazo zitaingia hatua ya 16 bora.

Kuna klabu ambazo tayari zimetangulia katika hatua hiyo kama vile Real Madrid, Barcelona, PSG, Juventus, Man City, Bayern Munich na Zenit.

Kivumbi ni leo kwa Klabu ya Manchester United ambayo itashuka dimbani dhidi ya Wolfsburg katika kundi B, huku kila timu ikihitaji ushindi ili kujihakikishia inaingia 16 bora.

Wolfsburg wanaongoza kundi hilo wakiwa na alama 9 wakati United ikiwa na alama 8 ikifuatiwa na PSV yenye alama 7.

Kama United itapoteza mchezo itawapa nafasi PSV endapo itashinda katika mchezo wake dhidi ya CSKA Moscow, ambapo wakishinda PSV itakuwa na alama 9, hili ni kundi gumu kwa timu hizo kutokana na tofauti ya alama.

Katika kundi C, kazi itakuwa nyepesi kwa timu ya Benfica na Atletico Madrid, hapa timu zote zina
alama 10 katika kundi lao.

Timu hizo zinafuzu hatua ya 16 kwa kuwa wapinzani wao kwenye kundi hilo Galatasaray wana alama 4 wakati huo Astana wakiwa na alama 3, ambapo itakuwa ngumu kwao kufuzu katika michezo yao ya leo.

Michezo mingine ambayo itapigwa leo ni pamoja na Man City ikipambana na Monchengladbach, Real Madrid dhidi ya Malmo, Sevila dhidi ya Juventus, huku PSG ikicheza dhidi ya Shakhtar.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles