27.5 C
Dar es Salaam
Sunday, December 3, 2023

Contact us: [email protected]

Van Gaal kuongezewa mkataba mpya United

Van GaalMANCHESTER, ENGLAND

KLABU ya Manchester United inatarajia kufanya mazungumzo na kocha wake Louis van Gaal kwa ajili ya
kumuongezea mkataba mpya Januari mwakani.

Uongozi wa klabu hiyo umesema una furaha kubwa kuwa na kocha huyo tangu alipoanza kuiongoza miezi 17
iliyopita.

Van Gaal alijiunga katika klabu hiyo kwa mkataba wa miaka mitatu, hivyo mkatab huo unatarajia kumalizika
2017, hivyo makamu mwenyekiti wa klabu hiyo, Ed Woodward amedai kwamba wana imani na kocha huyo.

Hata hivyo, awali Van Gaal alisema kuwa baada ya kumaliza mkataba wake katika klabu hiyo atatangaza kustaafu kwa kuwa alimuahidi mke wake kuwa atafanya hivyo.

Lakini Man United bado inaamini kuwa itaweza kumshawishi kocha huyo kuendelea kukaa katika klabu
hiyo.

Klabu hiyo kwa sasa inashika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi ikiwa na alama 29 sawa na wapinzani wao Manchester City ambao wanashika nafasi ya tatu wakitofautiana kwa mabao.

Hata hivyo, Van Gaal anaamini kuwa klabu hiyo ina nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye michuano hiyo msimu
huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles