27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Wangechi kuachia wimbo mpya na Ne-Yo

Wangechi na Ne YoNAIROBI, KENYA

MSANII wa muziki nchini Kenya, Wangechi Mutu, anatarajia kuachia wimbo wake mpya ambao amefanya na mkali wa RnB kutoka nchini Marekani, Ne-Yo.

Wimbo huo uliandaliwa tangu Agosti mwaka huu, hivyo unatarajiwa kuachiwa mwishoni mwa wiki hii huku jina likitarajiwa kutajwa wakati wa utambulisho wa wimbo huo.

“Wimbo ulikuwa tayari muda mrefu, lakini mambo hayakuwa sawa, ila kwa sasa kila kitu kimekamilika na hii ni wiki ya kuachia ngoma hiyo, jina la wimbo litajulikana wakati wa utambulisho,” alieleza Wangechi.

Ne-Yo alikuwa nchini Kenya kwa ajili ya tamasha la Coke Studio Africa, ambapo alifanya kazi na wasanii mbalimbali kutoka Afrika akiwemo Ali Kiba (Tanzania), Maurice Kirya (Uganda), Dama Do Bling (Msumbiji) na Ice Prince (Nigeria).

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles