27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 16, 2024

Contact us: [email protected]

Victoria: Sina mpango na wanaume wa Kenya

Victoria_KimaniNAIROBI, KENYA

MSANII wa muziki nchini Kenya, Victoria Kimani, amesema hana mpango wa kuolewa na wanaume wa nchini Kenya kwa kuwa hawajui kukaa na wapenzi wao.

Mrembo huyo amesema wanaume wengi wa nchini humo wamekuwa tofauti na wale wa nchini Nigeria, hivyo ni bora aelekee huko kwa ajili ya kupata mwanaume bora ambaye atadumu naye.

Msanii huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri katika muziki mara baada ya kusaini mkataba mpya katika kampuni ya kusimamia kazi zake ijulikanayo kwa jina la Chocolate City Music Label, amesisitiza kwamba lengo lake kubwa ni kuolewa na mtu kutoka Nigeria.

“Wanaume wa Nigeria wanajua jinsi ya kuishi na mwanamke, wanaonyesha heshima ya hali ya juu na hivyo ndivyo ninavyotaka katika maisha yangu,” alisema Victoria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles