CALIFORNIA, MAREKANI
Hatimaye wanandoa staa wa muziki wa RnB na filamu nchini Marekani, Tyrese Gibson na mke wake, Samantha Lee, wamefanikiwa kupata mtoto wa kwanza.
Tyrese ametumia ukurasa wake wa Instagram kuthibitisha kuzaliwa kwa mtoto wao wa kike ambaye wamempa jina la Soraya Lee Gibson.
“Mungu baba tunakupenda kwa kutuletea Soraya Lee Gibson ambaye ulituahidi, tunaamini maisha yetu kwa sasa yatakwenda kubadilika,” aliandika staa huyo wa muziki na filamu.
Mapema Aprili mwaka huu wawili hao walitangaza kupitia mitandao yao ya kijamii kuwa wanatarajia mtoto wa kike. Ndoa yao ilifungwa tangu siku ya wapendanao mwaka 2017, lakini ilikuwa ya siri.