25.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

Trump azuia safari za kutoka Ulaya kuingia nchini Marekani

WASHINGTON, MAREKANI

RAIS wa Marekani Donald Trump, ametangaza kuweka zuio kwa raia wa nchi za Ulaya kuingia nchini Marekani ili kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona.

Katika hotuba yake kwa njia ya Televisheni siku ya Jumatano, alisema safari zote za kutoka Ulaya zitazuiwa kwa siku 30 zijazo.

Lakini amesema ”hatua kali zilizo na umuhimu” hazitaihusisha Uingereza, ambayo ina visa 460 vya virusi vilivyothibitishwa.

Kuna visa 1,135 vilivyothibitishwa nchini Marekani na watu 38 wameripotiwa kupoteza maisha.

”Kuzuia visa vipya kuingia Marekani, tutaahirisha safari zote kutoka Ulaya,” Trump alieleza.

”Hatua hii itaanza kutekelezwa kuanzia usiku wa siku ya Ijumaa”. Aliongeza.

Trump amesema Umoja wa Ulaya umeshindwa kuchukua hatua za tahadhari kama hizo zilizoanzishwa na Marekani.

Alizungumza saa kadhaa baada ya Italia nchi iliyoathirika zaidi baada ya China kutangaza kuchukua hatua kali.

Hatua hizo ni pamoja na kufunga maduka yote isipokuwa yanayouza vyakula na dawa kama sehemu ya kujitenga.

Trump amesema kuahirishwa kwa safari pia kutahusu biashara na usafirishaji wa mizigo kutoka Ulaya kuingia Marekani.

Pia ametangaza kutoa mkopo wa mabilioni ya dola kwa wafanyabiashara wadogo, na kutaka bunge la Congress kupitisha nafuu ya kodi ili kukabiliana na athari za mlipuko wa corona kiuchumi.

HALI ILIVYO MAREKANI

Maofisa wamesema hatari ya maambukizi ilikuwa chini, lakini hali ilibadilika baada ya ongezeko la idadi ya visa vipya vya maambukizi vilivyothibitishwa mwanzoni mwa mwezi Machi.

Jitihada za kudhibiti zimeanza. Vikosi vimepelekwa kwenye mji wa New Rochelle, ulio kaskazini mwa New York, ambapo mlipuko huo unaaminika kuanzia huko.

Vikosi vya ulinzi vitatoa chakula kwa baadhi ya watu ambao wametakiwa kujiweka karantini.

Gavana wa jimbo la Washington amepiga marufuku mikusanyiko katika kaunti kadhaa. Jimbo lililo Kaskazini Magharibi ni kiini cha maambukizi nchini Marekani, kukiwa na idadi ya vifo 24 kati ya 38 nchi nzima.

Mkuu Shirika la Afya Duninai (WHO), Dk. Tedros Adhanom Ghebreyes ametangaza mlipuko wa Corona kuwa janga la kimataifa

Shirika la Afya duniani limeutangaza mlipuko wa virusi vya corona kuwa ni janga la kimataifa, huku mlipuko huo ukiendelea kusambaa katika mataifa mbalimbali duniani.

Ghebreyesus amesema kuwa idadi ya visa nje ya China vimeongezeka mara 13 kwa kipindi cha majuma mawili yaliyopita.

Amesema kuwa ana hofu kubwa kutokana na viwango vya maambukizi ya virusi.

Janga ni ugonjwa ambao unasambaa katika nchi nyingi kote duniani kwa wakati mmoja.

ITALIA

Waziri Mkuu, Giuseppe Conte alitangaza ongezeko la masharti ya kujiweka karantini kuongezeka.

Alisema maduka mengi, migahawa, saluni, vitafungwa hadi Machi 25.

Italia ina watu 12,000 waliothibitika kuambukizwa na idadi ya waliopoteza maisha ni 827. Karibu watu 900 wenye maambukizi wako kwenye hali mbaya, WHO imesema.

Wakati huo huo Saudi Arabia imesitisha kwa muda usafiri wa raia wake na wakaazi wengine na kuzuia safari za ndege kwenda katika mataifa kadhaa kutokana na hofu ya virusi vya Corona.

Shirika la habari la nchi hiyo SPA lilisema jana na kutaja chanzo rasmi katika wizara ya mambo ya ndani.

Uamuzi huo unajumuisha mataifa ya Umoja wa Ulaya, Uswisi, India, Pakistan, Sri Lanka, Ufilipino, Sudan, Ethiopia, Sudan Kusini Eritrea, Kenya, Djibouti na Somalia,

chanzo hicho kimeongeza, kikisema Uingereza pia imesitisha kuingia nchini humo kwa wale watu wanakuja kutoka nchi hizo.

Saudi Arabia pia imesitisha kwa muda usafiri wa abiria na pia kwa njia ya barabara na Jordan, wakati usafirishaji wa mizigo na biashara vinaruhusiwa bado, na usafirishaji wa abiria wenye uhitaji maalum wa kiutu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles