30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

TRUMP ATAKA BUNGE LITOE MISAADA KWA MARAFIKI WA MAREKANI PEKEE

WASHINGTON, MAREKANI


AKICHOCHEWA na hasira za upinzani ulioonyeshwa na jumuiya ya kimataifa juu ya kutambua kwake Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel, Rais Donald Trump, amelitaka Bunge la Marekani kuelekeza misaada ya kigeni kwa ‘marafiki wa Marekani’ pekee.

Kauli ya Trump, ikiwa ni sehemu ya hotuba yake ya kwanza kwa taifa aliyoitoa usiku wa kuamkia jana, ambayo ilishangiliwa bungeni na wabunge wa chama chake cha Republicans na kupuuzwa na wale wa Democrats, inaweza kuiweka Marekani katika sintofahamu na washirika wake muhimu, ambao wamekosoa uamuzi wake.

Kauli ya Trump inatokana na uamuzi wa Desemba 22 mwaka jana wakati mataifa 128 katika mkutano wa Umoja wa Mataifa yalipopiga kura kuitaka Washington ibatilishe uamuzi wa kuitambua Jerusalem.

Alisema mataifa hayo yaliyoipinga yalipokea jumla ya dola bilioni 20 kama msaada kutoka Marekani mwaka 2016.

“Ndiyo maana, usiku huu ninalitaka Bunge kupitisha sheria kuhakikisha msaada wa kigeni daima unatumika kwa masilahi ya Marekani na kwenda tu kwa marafiki zetu badala ya maadui zetu,” alisema.

Jumuiya ya kimataifa iliukataa uamuzi wa Trump kwa sababu Jerusalem inachukuliwa kama moja ya masuala magumu zaidi, ambayo yanapaswa kuwa ya mwisho kimajadiliano katika mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati.

Israel inadai Jerusalem kuwa mji wake mkuu wakati Wapalestina wanauona upande wa Jerusalem Mashariki kuwa mji mkuu wa taifa lao la baadaye.

Iwapo tishio la misaada la Trump litapitishwa, litaleta sintofahamu na washirika wake wakubwa, ambao ni wapokeaji wakuu wa misaada ya kiuchumi na kijeshi.

Miongoni mwao ni Afghanistan, Misri, Jordan na Pakistan, ambazo zote zilipiga kura kupitisha azimio hilo.

Misaada hiyo imelenga kuleta utulivu katika Serikali hizo zinazokabiliwa na wanamgambo wenye itikadi kali.

Pakistan kwa mfano, ingawa imekuwa ikikasirisha tawala nyingi za Marekani, zilishindwa kuitosa zikihofia silaha za nyuklia za taifa hilo kuangukia mikononi mwa wanamgambo wenye nia mbaya.

Tayari Marekani imezuia kiasi cha dola milioni 65 kati ya milioni 125 za msaada kwenda Palestina, hatua ambayo imesababisha maandamano miongoni mwa Wpalestina.

Mataifa mengine yatakayoathirika na tisho la Trump ni kutoka Afrika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles