Washington, Marekani
MWENDESHA mashtaka wa Marekani, Preet Bharara (46) amefukuzwa kazi na Rais Donald Trump.
Bharara aliteuliwa na Rais aliyetangulia, Barack Obama, alishauriwa na Naibu Mwanasheria Mkuu kujiuzulu.
Mwendesha mashtaka huyo alikataa kujiuzulu, baada ya kuambiwa binafsi na Trump, baada ya uchaguzi mkuu wa urais Novemba mwaka jana.
Kupitia mtandao wa jamii wa Twitter, Bharara, ameandika kuwa hajajiuzulu bali amefukuzwa kazi.
"Kutumikia nchi yangu ya Marekani kama mwanasheria kwa miaka saba imekuwa heshima kubwa ya maisha yangu na taaluma.
“Bila kujali nitafanya nini au muda gani nitaishi ," Bharara alisema hayo katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.