31.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Tumejipanga kuimarisha utalii wa Malikale- CC DKT. DORIYE

Na Mwandishi wa NCAA.

Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) Dkt. Elirehema Doriye amesema Mamlaka hiyo imejipanga kuhakikisha inalinda, inahifadhi na inaimarisha vivutio vya malikale inavyovisimamia.

Akizungumza mara baada ya kutembelea Mapango ya Amboni mkoani Tanga yanayosimamiwa na Mamlaka hiyo Dkt.Doriye amesema mapango ya Amboni ni moja ya vituo vya malikale ambayo NCAA imedhamiria kuhifadhi, kuendeleza, kuboresha na kuyatangaza zaidi ili kuongeza idadi ya wageni wanaotembelea mapango hayo.

“ziara yangu katika mapango haya ni sehemu ya hatua za kuimarisha eneo hili ili kuongeza chachu katika utalii wa malikale, juhudi kadhaa tumeshafanya katika eneo hili ikiwepo uboreshaji wa njia za kupita ndani ya mapango, kuwekea taa ndani ya mapango, tunaendelea na ujenzi wa geti, kuimarisha mifumo ya malipo na kuongeza Ulinzi wa eneo lote la mapango, ,”alisema Dkt.Doriye

Dkt. Doriye ameongeza kuwa kwa sasa NCAA inaendelea kutanua wigo wa mazao mapya ya utalii ili kuongeza vyanzo vya mapato na kuongeza mtawanyiko wa wageni hasa katika vituo vya malikale.

“Tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na wizara yetu kwa kutuongoza vizuri katika kusimamia sera na mipango yetu ya kuongeza vyanzo vya utalii na Mamlaka haitowaangusha viongozi wetu hao,”alisema Dkt.Doriye.

Mapango ya Amboni yamebeba historia kubwa ya harakati za kudai uhuru ambapo inaelezwa kuwa baadhi ya wapinga ukoloni waliyatumia katika harakati za kudai uhuru wa Nchi.

Mapango ya Amboni ni moja ya vituo vya malikale vinavyosimamiwa na NCAA ambapo vituo vingine ni eneo la Engaruka lililoko Monduli, Majabali ya Mumba yaliyopo Karatu, Kimondo cha Mbozi Songwe pamoja na makumbusho ya bonde la Olduvai lililopo Ngorongoro.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles