25 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

TRA Kilimanjaro watakiwa kuwa wabunifu

Na Upendo Mosha, Moshi

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai, ameiagiza Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) mkoa wa Kilimanjro, kuwa wabunifu katika ukusanyaji wa kodi na kuthibiti mianya ya upotevu wa mapato katika vituo vyote vya forodha.

Pia Kagaigai amewatahadharisha wafanyabishara kuacha kutumia njia za maghendo katika uvushaji wa bidhaa zao mipakani na badala yake kutumia njia halali ili kukwepa kuvunja sheria za nchi.

Kagaigai alitoa agizo hilo jana kwa uongozi wa TRA mkoani Kilimanjaro, wakati wa ziara yake ya kikazi ya kutembelea ofisi hiyo na vituo vya forodha katika wilaya za Moshi, Hai, Siha na Rombo.

Alisema licha ya mamlaka hiyo kujitahadi katika ukusanyaji wa mapato bado jitihada zaidi zinahitajika katika ubunifu na kuthibiti mianya ya upotevu wa mapato jambo ambalo litasaidia kuvuka malengo ya ukusanyaji.

“TRA mkoa wa kilimanjaro mnawajibu wa kubuni vyanzo vingi vya mapato na kutoa elimu kwa walipa kodi ili waelewe nini faida ya kulipa kodi na nini hasara ya kutolipa kodi kwa jambo hili litaongeza wigo wa walipa kodi,”alisema Kagaigai.

Aidha, amesema wafanyabishara wanaokwepa kulipa kodi kwa kuficha bidhaa zao katika maghala ni kosa kisheria na ni uhujumu uchiumi na kwamba atakaye bainika kufanya hivyo mkono wa sheria hautamuacha salama.

“Wafanyabishara wanaoficha bidhaa zao stoo kwa lengo la kukwepa kodi hilo ni kosa la uhujumu uchumina sidhani kama vi vizuri…mfanyabishara ni mtu msitaara lakini akikwepa kufuata sheria atapoteza ustaarabu wake na ndio maana nimehimiza wafanyakazi wa (TRA) kuhakikisha wafanyabishara wanafuata sheria,”alisema.

Kwa upande wake Meneja wa (TRA) mkoa wa Kilimanjaro, Gabriel Mwangosi, alisema katika kipindi cha mwaka wa fedha 2020/2021 kuanzia Julai hadi Juni walijiwekea malengo ya kukusanya zaidi ya Sh blioni 226 na kufanikiwa kukusanya zaidi ya bilioni 193 ambapo ni sawa na aslimi 89 ya malengo.

Alisema sababu zilizochangia kushindwa kufikia malengo ya kukusanyaji kwa asilimia mia ni pamoja na kuzuka kwa ugonjwa wa corona,upungufu wa watumishi pamoja na upungufu wa baadhi ya vifaa na vitendea kazi.

“Mkoa wetu ni miongoni mwa mikoa inayotegemea utalii hivyo kuzuka kwa ugonjwa wa corana kumepelekea biashara nyingi kuyumba sana ambapo hata ulipaji wa kodi umetokea kukwama kwa baadhi ya wafanyabishara kufunga kabisa biashara zao,”alisema.

Mwangosi alisema pamoja na changamoto hizo wamejiweka mikakatika mbalimbali ya kuongeza mapato ikiwa ni pamoja na kuziba mianya ya uvujaji na upotevu wa mapato,kutoa elimu ya mlipa kodi na kusimamia vema mashine za kieletroniki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles