22.8 C
Dar es Salaam
Saturday, June 3, 2023

Contact us: [email protected]

Manara augeukia Muziki wa Bongo Fleva

Na Brighiter Masaki, Mtanzania Digital

Msemaji wa Mabingwa wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara Simba Sports Klabu, Haji Manara, ametangaza kumpa nafasi ya kuimba Msanii Chipukizi wa Bongo Fleva, Twisco katika Tamasha la Simba Day Agosti 8, 2021.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Dar es Salaam leo Jumatatu Julai 12, 2021, wakati wa kumtambulisha msanii huyo, aliyepo chini ya lebo ya Katemi Empire, Manara amesema niwakati wa kusapoti wasanii chipukizi.

“Tunatakuwa kuwasapoti wasanii chipukizi waweze kufikia nafasi za wasanii wakubwa, ili tuweze kuwa na kina Diamond na Ali Kiba wengi atawakishindana kimataifa tubafanya kuchagua tu.

“Twisco anaimba hivyo anahitaji kupewa ushirijiano na watanzania, binafsi ntahakikisha anaimba siku ya Simba Day na wengine chipukizi wataimba na msanii yoyote mkubwa atakaechaguliwa,” amesema Manara.

Kwa upande wake Twisco amesema anashukuru kwa ushirikiano ambao Manara amemuonyesha ushirijiani na Lebo yake ya Katemi Empire kwa kumtambulisha kwa watanzania anawaahidi kufanyakazi kwa bidii.

Aidha, amemshukuru msanii wa Bongo fleva Alikiba kwa kumtia moyo na ushirikiano anaompa kila anapokata tamaa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,270FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles