25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

TCU yafungua dirisha la kwanza la udahili kwa wanafunzi wa elimu ya juu

Na Brighiter Masaki, Dar es Salaam

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imefungua dirisha la kwanza la udahili kwa wanafunzi wa elimu ya juu (shahada ya kwanza) kwa mwaka wa masomo wa 2021/ 2022 huku ikianisha sifa zinazohitajika kwa wanafunzi kusoma katika vyuo vikuu mbali mbali nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, Dar es Salaam, Jumatatu Julai 12,2021 Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Charles Kihampa amesema hatua hiyo imekuja kufuatia kutangazwa kwa matokeo ya kidato cha sita Julai 10,2021.

Profesa Kihampa amesema, dirisha hilo limefunguliwa kuanzia leo Julai 12,2021 hadi Agosti 5,2021.

Amesema,udahili wa kujiunga na shahada ya kwanza utahusu waombaji waliohitimu wa kidato cha sita; wenye Stashahada (Ordinary Diploma); na waliomaliza programu ya ‘Foundation’ ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT).

Ili kufahamu sifa stahiki za kujiunga na Chuo Kikuu waombaji wameelekezwa kusoma vigezo vilivyopo kwenye vitabu vya muongozo vya TCU huku pia wakitakiwa kutuma maombi yao moja kwa moja kwenye vyuo ambavyo wamevichagua na kwamba maelekezo ya jinsi ya kutuma maombi yanayotolewa na vyuo vikuu husika.

Aidha Prof. Kihampa amewapa tahadhari waombaji wote wa shahada ya kwanza ikiwa watahitaji kupata ufafanuzi wa suala lolote juu ya udahili kuwasiliana moja kwa moja na vyuo husika ama TCU.

“Tunawaasa wananchi kuepuka kupotoshwa na watu wanaojiita mawakala au washauri wanaodai wanatoa huduma ya jinsi ya kujiunga na vyuo vya elimu ya juu hapa nchini,” amesema Prof. Kihampa.

Amesema masuala muhimu ambayo waombaji wanapaswa kuzingatia ni pamoja ma kusoma muongozo wa udahili na kuuelewa, kuingi kwenye tovuti za vyuo ili kujua taratibu za kutuma maombi, kutuma maombi moja kwa moja vyuoni kupitia mifumo ya kielektoniki na kuwasiliana na vyuo ili kupata taarifa huku pia waombaji wenye vyeti vinavyoyolewa na NECTA au NACTE wakitakiwa kupata idhibati ya ulinganifu wa sifa zao kabla ya kutuma maombi ya udahili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles