Na JENNIFER ULLEMBO-DAR ES SALAAM
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Ally ‘Timbulo’, ameeleza kuwa anatoa nafasi kwa mashabiki kumpangia kazi wanazotaka kuzisikiliza kwa mwaka huu.
Akizungumza na MTANZANIA, Timbulo alisema ametoa nafasi hiyo ili kuwapa moyo na fusra ya kuchagua kile wanachokipenda.
Timbulo alisema kila mara wasanii wamekuwa wakifanya kazi zao bila kuwashirikisha mashabiki na wadau wa muziki.
“Natoa nafasi kwa mashabiki wachague mwaka huu tuanze na nyimbo gani, maana kila mara nimekuwa nikifikiria mimi tu,” alisema Timbulo.
Msanii huyo alisema anaheshimu mawazo na mapendekezo ya mashabiki zake duniani, hivyo ni fursa kwake kuwasikiliza kwanza.