22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

TIMBULO AWAPA RUNGU MASHABIKI

Na JENNIFER ULLEMBO-DAR ES SALAAM


MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Ally ‘Timbulo’, ameeleza kuwa anatoa nafasi kwa mashabiki kumpangia kazi wanazotaka kuzisikiliza kwa mwaka huu.

Akizungumza na MTANZANIA, Timbulo alisema ametoa nafasi hiyo ili kuwapa moyo  na fusra ya  kuchagua kile wanachokipenda.

Timbulo alisema kila mara wasanii wamekuwa wakifanya kazi zao bila kuwashirikisha mashabiki na wadau wa muziki.

“Natoa nafasi kwa mashabiki wachague mwaka huu tuanze na nyimbo gani, maana kila mara nimekuwa nikifikiria mimi tu,” alisema Timbulo.

Msanii huyo alisema anaheshimu mawazo na mapendekezo ya mashabiki zake duniani, hivyo ni fursa kwake kuwasikiliza kwanza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles