V MONEY AJITABIRIA MEMA 2018

0
846

Na JENNIFER ULLEMBO


MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Vannesa Mdee ‘V money’, amesema  mwaka 2018 unaweza kuwa ni wa mafanikio kuliko miaka yote iliyopita.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mwanadada huyo ambaye hivi karibuni aliweza kuachia albamu yake mpya iliyopewa jina la ‘Money Monday’, alisema kuanza vizuri kwa kuuza albamu ni moja ya kiashirio cha mafanikio mwaka 2018.

“Nina imani mwaka huu utakuwa wa mafanikio zaidi, siwezi kusema kuwa miaka iliyopita sijafanikiwa hapana, kila mwaka umekuwa ukija kivingine.

“Hatua niliyoanza nayo mwaka huu inanipa moyo wa kufika mbali zaidi, ingawa najua changamoto zipo na lazima tukumbane nazo ili kujijenga zaidi,” alisema V money.

Mwanadada huyo amekuwa akilitangaza vema Taifa la Tanzania katika tasnia nzima ya muziki upande wa wanawake, baada ya kubahatika kujikusanyia tuzo na kufanya kazi na wasanii mbalimbali wa kimataifa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here