NANDY AANZA KUPATA DILI KIMATAIFA

0
1310

Na JESSCA NANGAWE-DAR ES SALAAM


MREMBO anayefanya vyema na ngoma ya Kivuruge, Faustine Charles ‘Nandy’,  ameanza kupata ofa za kufanya shoo za kimataifa.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Nandy ambaye alisema kwa kipindi kirefu alikuwa akitamani kupata nafasi ya kufanya shoo nje ya nchi, sasa anaona matunda ya kazi zake baada ya kupokea mialiko kadhaa kutoka nchi mbalimbali.

“Ni sehemu ya ndoto niliyoitamani kwa muda mrefu, unajua watu wanapoona kazi zako zinafanya vema, hapo ndipo mwanzo wa mafanikio uonekana, nashukuru wengi wameliona hilo na sasa hata mialiko nimeanza kuipata ya ndani na nje ya nchi,” alisema Nandy.

Alieleza  kuwa huu ni mwaka wake wa kuhakikisha anafanya vizuri kimataifa, kwani tayari amejiwekea misingi mizuri hapa nyumbani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here