31.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

TGNP yawafunda wakurugenzi bajeti mrengo wa  jinsia

Na MWANDISHI WETU-MOROGORO

SERIKALI kupitia wizara zake zimeshauriwa kuhakikisha inatenga bajeti zenye mrengo wa  jinsia  ili kufikia lengo la kuwa na uchumi wa kati utakaowashirikisha wanawake na wanaume.

Mwenyekiti wa  Bodi ya Mfuko wa wanawake Tanzania,  Profesa Ruth Meena alikuwa akizungumza kwenye  kikao kazi cha  wakurugenzi wa mipango na sera kutoka wizara mbalimbali kilichoandaliwa na TGNP Mtandao  kwa kushirikiana na Shirika la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA).

Alisema  Serikali   inapaswa kuhakikisha kila bajeti   inazingatia usawa wa jinsia kwa kuwapa kipaumbele wanawake  kama ilivyo kwa wanaume.

Alisema   bajeti inayozingatia usawa huo ndiyo njia mojawapo  itayoiwezesha nchi kufikia kafikia malengo ya  mkakati ikiwamo   ya kuhakikisha ifikapo mwaka 2020 -2025  unanyanyasaji wowote  wa  jinsia umekuwa umetoweka.

Profesa Meena alisema lengo ilkiwa ni kuondoa ubaguzi hususan kwa wanawake kama sehemu ya kutekeleza Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili wa Jinsia kwa Wanawake na Watoto (NPA) ifikapo 2022.

“Kwa kiupindi cha zaidi ya miaka 25, TGNP tumesimamia eneo la bajeti ya mrengo wa jinsia, leo (juzi) siyo mara ya kwanza kukaa na watu wa serikali.

“Tunakutana na watendaji wa serikali kwa ngazi tofauti hadi makatibu wakuu, kuhakikisha  wanaelewa masuala ya jinsia na kuyazingatia wakati wa kuandaa mipango yao na sera za nchi.

“Ni lazima pia jamii kutambua masuala ya jinsia  ni uwiano sawa kati ya mwanamke na mwanamume katika nyanja zote,’’ alisema Profesa Meena

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao,  Lilian Liundi alisema    baada ya kugundua baadhi ya wizara  bajeti zake zilikuwa hazilengi moja kwa moja usawa wa  jinsia, TGNP imeweza kukutana na wakurugenzi wa wizara mbalimbali    kujadili umuhimu wa kupanga bajeti kwa kuzingatia usawa wa jinsia.

“Endapo serikali  italiwekea mkazo zaidi suala hili la usawa wa jinsia katika bajeti zake nitasaidia kuongeza uwajibikaji  na matumizi  mazuri za rasilimali za nchi kwa sababu mwanamke atakuwa amehusishwa moja kwa moja katika  bajeti hiyo bila kubaguliwa,” alisema Liundi.

Akifungua rkikao hicho, Mkurugenzi Msaidizi  kutoka Idara  ya Jinsia sehemu ya wanawake kutoka Wizara ya afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mboni Mgaza alisema wizara   imepewa jukumu la sera  la kuratibu masuala ya usawa wa jinsia na uwezeshaji wa wanawake.

 

TGNP Mtandao kwa kushirikiana Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Shirika la Idadi ya watu Duniani (UNFPA) wanatekeleza kwa pamoja mradi wa kuhakikisha serikali kuu na serikali za mitaa zinatenga fedha kwenye bajeti yake kwa ajili ya kuwezesha kutokomeza mila potofu na vitendo vya ukatili wa  jinsia nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles