31.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

TENGENI VYUMBA KUJIHIFADHI WANAFUNZI WA KIKE – WAZIRI

NA RAMADHAN HASSAN, DODOMA

WIZARA ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, imesema shule zinatakiwa kutenga vyumba maalum kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wa kike kujihifadhi wakati wa siku zao nzito.

Hayo yalisemwa bungeni jana na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Stella Manyanya, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum, Zaynabu Vullu (CCM), aliyetaka kufahamu serikali ina mpango wa gani wa kuwatengea wanafunzi hao wakati wa siku zao nzito.

Manyanya alisema suala la wanafunzi wa kike ni mtambuka,  hivyo ni lazima watoto watengewe sehemu maalum ya kujihifadhi wakati wa siku zao  na kupewa taulo maalum za kujistiri.

“Hili ni suala ambalo linafahamika, wanafunzi wa kike wanatakiwa kutengewa chumba maalum kwa ajili ya kujihifadhi wakati wa siku zao, pia hawa wanafunzi wanatakiwa wapatiwe taulo maalum (ped) ya kujistiri,” alisema Manyanya.

Katika swali la msingi, Vullu alitaka kufahamu serikali ina mpango gani wa kuwahakikishia wanafunzi wanaopata mimba wakiwa shuleni kuendelea na masomo baada ya kujifungua.

Akijibu, Naibu Waziri Manyanya, alisema sera ya elimu na mafunzo ya 2014 imeweka mkazo juu ya kuhakikisha upatikanaji wa elimu kwa wote.

“Sera inatamka wazi, serikali itaondoa vikwazo vinavyozuia fursa ya wanafunzi kuendelea na masomo ili kukamilisha mzunguko wa elimu katika ngazi husika na kuhakikisha usawa wa jinsia katika elimu na mafunzo unazingatiwa,” alisema.

Alisema sehemu ya utekelezaji wa sera hiyo serikali imeandaa rasimu ya muongozo utakaofuatwa na wadau mbalimbali kuwawezesha wasichana waliopata mimba kuendelea na masomo baada ya kujifungua.

Alisema pamoja na serikai kuondoa vikwazo kwa mtoto wa kike aweze kuendelea na masomo, wito unatolewa kwa wadau wakiwamo wazazi, walimu, viongozi wa elimu na dini, kudhibiti tatizo la mimba shuleni na wale wenye umri mdogo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles