33.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

TBA kuendesha operesheni ya kuwaondoa wadaiwa sugu Oktoba 7, 2024

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) umepanga kuendesha operesheni ya kuwaondoa wadaiwa sugu 648 katika mikoa ya Arusha, Mwanza, Dodoma, na Mara kuanzia Oktoba 7, 2024. Hatua hii inachukuliwa baada ya wadaiwa hao kushindwa kulipa malimbikizo ya madeni, licha ya kupewa notisi ya awali.

Mkurugenzi Mtendaji wa TBA, Arch Daud Kondoro, amesema kuwa wadaiwa hao wamepewa notisi ya wiki mbili na wanadaiwa jumla ya Shilingi bilioni 14.8. Wale watakaoshindwa kulipa madeni yao watafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

“Mikoa ya Dodoma, Arusha, Mwanza, na Mara inadaiwa jumla ya Sh bilioni 1.7. Tunawahimiza wateja wetu kulipa madeni mara baada ya kupokea ujumbe wa kumbukumbu ya malipo unaotumwa kila mwezi,” alisema Arch Kondoro wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

Katika juhudi za kuboresha ukusanyaji wa madeni, TBA imekabidhi jukumu la kuwaondoa wadaiwa hao sugu kwa dalali wa mahakama, Twins Action Mart. Pia, TBA imeanzisha mfumo wa kielektroniki wa Usimamizi wa Miliki za Serikali (GRMS) ambao utawezesha watumishi wa umma kulipa kodi moja kwa moja kutoka kwenye mishahara yao.

Aidha, TBA imeanza kufunga vitasa vya kielektroniki (smart locks) na mita za kielektroniki (smart meters) katika nyumba zao ili kuboresha usimamizi wa mali na ukusanyaji wa madeni kutoka kwa wapangaji.

Kwa sasa, wapangaji na wadaiwa sugu wanahimizwa kufuatilia taarifa zao kupitia tovuti na mitandao rasmi ya kijamii ya TBA ili kuepuka upotoshaji wa taarifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles