26.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Sumaye atoka hospitalini

sumaye1Na Veronica Romwald, Dar es Salaam

WAZIRI Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye aliyekuwa amelazwa katika Taasisi ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyoko Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), ameruhusiwa kurudi nyumbani.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Ofisa Uhusiano Msaidizi wa MNH, John Steven, alisema Sumaye aliruhusiwa juzi jioni baada ya madaktari kuridhishwa na maendeleo ya afya yake.

“Sumaye amepewa ruhusa ya kurudi nyumbani tangu juzi jioni, madaktari wake waliridhishwa na mwenendo wa afya yake kutokana na matibabu waliyompatia dhidi ya ugonjwa uliokuwa unamsumbua,” alisema.

Hata hivyo, Steven hakufafanua ugonjwa uliokuwa ukimsumbua kiongozi huyo mstaafu kwa kile alichoeleza kuwa kanuni na sheria za kitabibu zinakataza.

“Siwezi kutaja ugonjwa uliomfanya akalazwa hapa, mwenyewe anaweza kuwaeleza kwa sababu ni siri yake na daktari wake,” alisema.

Sumaye alilazwa hospitalini hapo Januari 7, mwaka huu na Januari 11, Rais John Magufuli, alimtembelea hospitalini hapo na kumpa pole.

Mapema mwaka huu, Sumaye alitangaza rasmi kujiunga na Chadema baada ya kuondoka katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka jana muda mfupi kabla ya kampeni za uchaguzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles