27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Ufaulu kidato cha pili washuka

necta* Hisabati, Fizikia, Baiolojia, Kiingereza na Biashara hali mbaya
*Mwanza na Dar zachuana 10 bora, Mtwara, Tanga na Lindi hoi

NA VERONICA ROMWALD, DAR ES SALAAM

KIWANGO cha ufaulu cha wanafunzi waliofanya mtihani wa upimaji wa kitaifa wa kidato cha pili (FTNA) mwaka jana kimeshuka kutoka asilimia 92.66 hadi kufikia 89.12.
Hayo yameelezwa jana na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Dk. Charles Msonde, wakati akitangaza matokeo ya mitihani hiyo katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyikia ofisini kwake Dar
es Salaam.

Alisema mtihani huo uliofanyika Novemba 16 hadi 27, mwaka jana, jumla ya wanafunzi 396,770 waliandikishwa
huku wasichana wakiwa 199,615 sawa na asilimia 50.31 na wavulana ni 197,155 sawa na asilimia 49.69.

Dk. Msonde alisema wanafunzi 33,104 sawa na asilimia 8.34 hawakufanya mtihani kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo utoro na ugonjwa na 39,567 sawa na asilimia 10.88 hawakufaulu hivyo watarudia kidato cha pili.

“Kati ya wanafunzi hao walioandikishwa, 324,068 sawa na asilimia 89.12 pekee ndiyo waliopata ujuzi na maarifa ya kuwawezesha kuendelea na kidato cha tatu, wasichana wakiwa 164,547 sawa na asilimia 89.00 na wavulana 159,521 sawa na asilimia 89.24.

“Idadi ya watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa madaraja ya ‘Dinstinction, Merit na Credit’ ni 155,667 sawa na asilimia 42.80 wakiwemo wasichana 68,780 sawa na asilimia 37.20 na wavulana 86,887 sawa na asilimia 48.60,” alisema Dk. Msonde.

Alisema ufaulu katika masomo ya msingi ya Kiswahili, Kemia na ‘Commerce’ umepanda kidogo ikilinganishwa na mwaka jana huku ufaulu kwa masomo ya Uraia, Historia, Jiografia, Fizikia, Biolojia, Kiingereza na Biashara ukishuka.

“Katika mtihani huo wanafunzi wamefaulu zaidi somo la Kiswahili kwa asilimia 86.34 lakini kwa upande wa somo la hisabati ufaulu upo chini zaidi kwa asilimia 15 mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana,” alisema Dk. Msonde.

Aliyataja masomo mengine ambayo ufaulu wake upo chini ya wastani ni Fizikia, Kemia na Biashara na kwamba juhudi za makusudi zinahitajika ili kuinua kiwango cha ufaulu kwa masomo hayo.

Aidha, alisema wanafunzi 31 walibainika kufanya udanganyifu katika mitihani yao hivyo matokeo yao yalifutwa.
Akizungumzia shule zilizofanya vizuri, alizitaja shule kumi bora kuwa ni Mwanza Alliance, Alliance Girl’s, Alliance Rock Army zote za mkoani Mwanza, St. Francis Girls ya Mbeya, Bethel Sabs Girl’s ya Mafinga mkoani Iringa, Don Bosco Seminary ya Iringa na Shamsiye Boy’s, Feza Boy’s, Feza Girls, Canossa za Dar es Salaam.

Pia alizitaja shule kumi zilizofanya vibaya kuwa ni Michenjele, Mkoreha na Makong’onda za mkoani Mtwara, Furaha
ya Dar es Salaam, Mdando, Mlongwema, Kwai, Mlungui na Kwalugulu zote za Mkoa wa Tanga na Lionja ya Lindi.

“Wanafunzi waliofanya vizuri zaidi kwa kuangalia wastani wa pointi (GPA) ni Lineth Chrstopher wa St Aloysius Girl’s, Jerry Panga wa Marian Boy’s na Rhobi Simba  wa Marian Gir’s za mkoani Pwani, Colin Emmanuel, Fuad Thabit wa Feza Boy’s, Geraldina Kyanyaka wa Canossa ya Dar es Salaam, Nickson Maro wa Magnificat ya Kilimanjaro, Diana Mwakibinga wa Morning Star, Elisha Peter, Buswelu na Gaudence Lwitakubi wa Alliance Girl’s za Mwanza,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles