28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yazifunga redio 28

mbarawaNA ESTHER MNYIKA, DAR ES SALAAM

SERIKALI imezifungia redio 28  kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo  kushindwa kulipa ada za leseni na kutimiza masharti yaliyowekwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Professa Makame Mbarawa, alisema majina ya redio zilizofungwa yatatangazwa baadaye na TCRA.

“Natoa agizo kwa kampuni mbalimbali kulipa ada za leseni kwa wakati ambao umepangwa na TCRA na ambao hawatatekeleza agizo hilo watachukuliwa hatua za kisheria,” alisema Profesa Mbarawa.

Wakati huo huo, Serikali imeifungia Kampuni ya Six Telecom Tanzania Limited kutokana na kudaiwa Sh bilioni 7.2.

Waziri Mbarawa alisema kampuni hiyo imebainika kufanya makosa mbalimbali ikiwemo kushindwa kulipa ada za leseni zenye thamani ya Sh bilioni moja.

Profesa Mbarawa alisema kwa sababu hizo Serikali imeifunga kampuni hiyo na tayari imewafikisha polisi baadhi ya watumishi wake kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles