Gabriel Mushi na Ramadhani Hassan, Dodoma |
MJADALA wa Sukari, uhaba wa mafuta ya kula na ukosefu wa maji katika majimbo mbalimbali, umetikisa Bunge huku Spika wa Bunge, Job Ndugai, akitoa maagizo mazito kwa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage.
Mjadala wa sukari uliibuka baada ya Mwijage kujibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mpendae, Salim Hassan Turky (CCM).
Katika swali la msingi lililoulizwa na Mbunge wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BWL), Jaku Hashim Ayoub, alihoji utofauti wa bei ya sukari katika pande mbili za muungano ambapo alisema gunia moja la kilo 50 linauzwa kwa Sh 65,000 Zanzibar wakati bara linauzwa kwa Sh 120,000.
Akijibu swali hilo, Mwijage alisema asilimia 53 ya sukari inayotumika Zanzibar huagizwa kutoka nje kwenye vyanzo ambavyo gharama zake ni nafuu ikilinganishwa na asilimia 29 ya sukari inayoagizwa nje kwa upande wa Tanzania bara.
Alisema Tanzania bara haina uhaba wa sukari na kuwatoa hofu Watanzania kuelekea mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
“Katika kipindi cha mwezi Machi hadi June mwaka huu serikali kwa kuzingatia maoni ya wadau imetoa vibali vya kuingiza sukari tani 135,610 kwa kutoza ushuru pungufu kwa kiwango cha asilimia 25 badala ya asilimia 100,” alisema.
Alisema Serikali imechukua uamuzi wa kuhamasisha na kusimamia kampuni kubwa nne zinazozalisha sukari ili zipanue uwezo wa mashamba na viwanda vyao.
Aidha, katika swali la nyongeza Turky alisema licha ya waziri kutoa majibu mazuri ila kuna swali la msingi amelikimbia.
“Kwamba Zanzibar kuna …
Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.