27.7 C
Dar es Salaam
Saturday, June 10, 2023

Contact us: [email protected]

MBUNGE CCM ADAI KUGAWANA MIRADI ‘KIMJOMBA MJOMBA’ KUMEWAKOSESHA MAJI

Gabriel Mushi, Dodoma

Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ali Mohamed Kessy amesema anao ushahidi wa baadhi ya viongozi wakubwa waliomilikishwa miradi ya maji katika Mkoa wa Rukwa namna wanavyomshawishi ili asizungumze kuhusu ubadhirifu uliopo katika miradi hiyo.

Aidha, amesema kutokana na wakandarasi kupewa miradi kimjomba mjomba imesababisha wananchi wa Nkasi kukosa maji na kipindi cha masika huchimba maji kwenye madimbwi kama panya.

Kessy ametoa kauli hiyo leo Mei 8, bungeni jijini Dodoma wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji ambapo pamoja na mambo mengine amesema viongozi hao wanapewa zabuni za miradi hiyo kiujanja ujanja.

“Awamu ya nne mkandarasi alipewa mabilioni ya fedha, miaka kadhaa sasa bwawa halina maji, wizara inaibiwa hela… na viongozi wakubwa ndiyo wenye miradi, kwa ushahidi wananitafuta ili nizungumze nao nawakatalia, eti mbunge nyamaza, ili waibe zaidi?” amesema.

Pamoja na mambo mengine, amesema katika mkoa huo kumejitokeza ujambazi kwa wakandarasi wa miradi ya maji katika baadhi ya vijiji vya Nkasi ambao hata Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Isack Kamwelwe na Naibu wake, Juma Aweso waliona namna serikali inavyoibiwa fedha.

“Mradi wa Kamwala, mkandarasi ameingia mkataba wa Sh bilioni 7.7 wakati uwezo mdogo, anao uwezo wa kutekeleza miradi ya thamani ya Sh 750 lakini akapewa kijomba mjomba.

“Maelezo bodi ya usajili wa wakandarasi yalieleza kuwa mkandarasi huyu hana sifa, Baraza la Madiwani Nkasi lilimkatalia lakini akapewa kimjomba mjomba,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,414FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles