26 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

Sudan yapigwa ‘stop’ Umoja wa Afrika

ADIS-ABABA- ETHIOPIA

UMOJA wa  Afrika umeipiga marufuku Sudan kushiriki katika shughuli zozote za Muugano huo hadi hapo itakapounda serikali ya mpito inayoongozwa na raia.

Uamuzi huo umekuja baada AU kuwapatia watawala wa kijeshi wa taifa hilo siku 60 kukabidhi mamlaka kwa raia vinginevyo wapigwe marufuku.

AU imekuja na uamuzi huo mkubwa  baada ya utawala wa jeshi nchini humo kupuuza makubaliano ya awali ya kujiuzulu katika kipindi cha siku 15 kilichoafikiwa na AU Aprili 15 mwaka huu.

Baraza la amani na usalama la AU limesema kuwa limesikitishwa na hatua ya jeshi hilo kushindwa kukabidhi mamlaka kwa utawala wa raia hivyo linawapatia wanajeshi muda wa siku 60 kufanya hivyo.

Wakati AU ikitoa uamuzi huo wiki hii baada ya kuzuka vurugu jeshi lilitangaza kuvunja makubaliano ya awali ya kuendelea kusalia madarakani kwa miaka mitatu na badala yake limeitisha uchaguzi ufanyike ndani ya miezi tisa.

Wakati huohuo maafisa nchini Sudan kwa mara ya kwanza wamethibitisha kuwa hali nchini humo si nzuri lakini wamekanusha madai kuwa watu 100 kuuawa na wanajeshi wakati wa maandamano.

Maafisa hao wamekiri kuwa watu waliouawa ni 46 na si 100 kama inavyosemwa.

Wakati maofisa wakisema hivyo, madaktari wanadai kuwa vifo vinavyohusishwa na v vuguvugu la waandamanaji wiki hii imepanda na kufikia zaidi ya watu 100.

Walisema miili 40 iliopolewa kutoka mto Nile mjini Khartoum siku ya Jumanne.

Awali mamlaka ilikuwa kimya kuhusiana na suala hilo lakini,maafisa wa wa wizara ya usalama mapema jana walisema idadi ya waliyofariki ni 46.

Wakati huo huo wanaharakati wa upinzani nchini Sudan wamekataa wito wa kufanya mazungumzo na baraza la kijeshi kwa maelezo kuwa baraza haliwezi kuaminika baada ya msako wa nguvu dhidi ya waandamanaji.

Wakaazi wa Khartoum  wameiambia BBC kuwa wanaishi kwa uwoga.

Naibu mkuu wa Baraza hilo la Jeshi amepinga madai ya ukandamizaji na kuongeza kuwa wahalifu na walanguzi wa dawa za kulevya walikuwa wamejipenyeza katikati ya waandamanaji hao kufanya biahara zao.

“Hatutakubali vurugu kutokea na kamwe hatutarejea nyuma katika msimamo wetu. Hatuwezi kurudi nyuma. Lazima tuhakikishe nchi inaongozwa kwa utawala wa sheria,” alisema Mohammed Hamadan – ambaye pia anafahamika kama Hemedti  juzi wakati akizungumza moja kwa moja kupitia televisheni ya Taifa.

Ripoti kadhaa kutoka mjini Khartoum zinaeleza kuwa kikosi maalum cha kijeshi kinachojulikana kama Rapid Support Forces (RSF), kimekuwa kikifanya msako katika barabara kadhaa za mji huo na kinawalenga raia.

Kikosi hicho zamani kilijulikana kama wanamgambo wa Janjaweed, na kinasadikiwa kuhusika na mauji na ukatili katika mzozo wa Darfur Magharibi mwa Sudan mwaka 2003.

Vurugu zilizoshuhudia watu wakiuawa wiki hii zilianza baada ya maafisa wa usalama kupelekwa makao makuu ya kijeshi kwa ajili ya kuwaondoa waandamanaji siku ya Jumatatu.

Sudan imekua chini ya utawala wa kijeshi tangu Rais Omar al-Bashir alipopinduliwa mwezi Aprili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles