Suala la mifuko ya jamii ni muhimu katika uchumi wa kileo na Tanzania kama nchi inazingatia uweko wa mifuko hiyo na imeunda Mamlaka ya Mifuko ya Jamii (SSRA) ili kuisimamia mifuko hiyo kwa kuiendesha kwa ufanisi unaotakikana.
Wajibu wa SSRA kuundwa kwake mwaka 2008 kutokana na kifungu cha 5(i) cha sheria ya Mamlaka ni Usimamizi wa Sheria ya Hifadhi ya Jamii ni pamoja na kusajili mifuko, Watunzaji na Meneja wa Uwekezaji katika sekta ya Hifadhi ya Jamiii, kudhibiti, kurekebisha na kusimamia utendaji wa mifuko, watunzaji na mameneja wa Uwekezaji na kutoa miongozo kwa ajili ya usimamizi na uendeshaji wa sekta ya hifadhi ya jamii na kutetea kwa kulinda maslahi ya wanachama.
Kazi nyingine ni kusajili na kusimamia wasimamizi katika sekta ya hifadhi ya Jamii na kumshauri Waziri juu ya Sera na masuala ya kiutendaji yanayohusiana na Sekta ya Hifadhi ya Jamii.
Masuala mengine ni kutoa muongozo kwa mifuko , watunzaji kumbukumbu na Mameneja wawekezaji.
SSRA inasimamia mageuzi ya Sekta ya Hifadhi ya Janii kwa kuanzisha mafunzo, kushauri, kuratibu na kutekeleza mabadiliko ya sheria katika Sekta ya Hifadhi ya Jamii na vilevile kumteua msimamizi wa Mifuko pale inapobidi .
Lakini SSRA inatakiwa kurahisisha upanuzi wa wigo wa Hifadhi ya Jamii kuwafikia wale ambao bado hawajafikiwa ikiwa ni pamoja na makundi/ sekta zisizo rasmi na kuendesha mipango ya elimu na uhamasishaji kwa umma juu ya masuala ya hifadhi ya Jamii.
“Kwa kutekeleza masuala hayo nyeti inahitaji mipango thabiti na kuzingatia mwenendo usiotiliwa shaka na hivyo kuwa na uadilifu, utendaji kazi wa pamoja , ubunifu na usiri kwa kuhakikisha kuwa na siri kwq wadau wake kwa taarifa na maoni yoyote ya binafsi kwenye masuala nyeti yanabaki kuwa siri, “ anasema Irene Kisaka Mkurugenzi Mkuu wa SSRA.
SSRA inatakiwa kuwa na weledi kwa kufanya na kuwatumia wataalamu waliobobea kwa kuweka miongozo mahiri itakayowezesha kulinda maslahi ya wanachama na utoaji huduma bora za Hifadhi ya Jamii na hivyo kutoa huduma zinazolenga mteja kwa kuwatambua kote waliko ja kuwafuata kutoa huduma stahiki..
Ikiwa na mwongozo ulioelezwa hapa kwa mapana SSRA imeanza kuona mmomonyoko wa madili kwenye mifuko baada ya kubaini kuwa baadhi ya mifuko imeanza kuwa na mapungufu kwa kuishi bila kuzingatia sheria ambayo kwa siku za karibuni kunaonesha gharama za uendeshaji na utawala kuzidi kiwango kilichoruhusuiwa cha asilimia 10 ya makusanyo ya mfuko husika na hivyo kuwa kinyume na taratibu.
SSRA imetoa mwongozo kuhusu suala la hilo na kutaka mifuko kurekebisha hali hiyo ndani ya miaka miwili ijayo ili mambo yaende sawa na wale ambao matumizi yao ni chini ya kiasi hicho na wanotaka kuongeza matumizi yao wtafanya hivyo kwa kuzingatia matumizi yasizidi kiasi cha asilimia 0.1 ya kipatochake cha makusanyo kwa mwaka.
Mamlaka inaweza kuondoa kikwazo hicho kwa kuzingatia mahitaji halisi ya mfuko au mifuko ili kuongeza ukuaji wa mfuko na kuongeza tija kwa maslahi makubwa ya wanachama na skimu hiyo kwa muda utakaopangwa na sio vinginevyo.
Mkurugenzi wa SSRA wa masuala ya Sheria, Ornorius Njole amesema mwaka huu mwezi Julai kuwa mwongozo wa kuendesha mifuko umetolewa na umeanza kutumika kufuatia kuzidi kwa uvunjaji wa taratibu kwa baadhi ya mifuko kuhusu matumizi.
Njole alisema hayo wakati wa mkutano na Wahariri jijini akiwafahamisha maendeleo mbalimbali ya Mamlaka na kutoa maelezo muafaka juu ya kutokuwepo kwa fao la kujitoa katika huduma za mifuko ya jamii jambo tete kwa baadhi ya wanachama haswa wa migodini.
Amesema badala ya fao la kujitoa kuna fao la kukosa ajira na linatakiwa kuziba pengo la watu kukosa kipato na akasema mafao yataanza kutumika karibuni na huku utafiti utafanyika kwa kina kujua kwa nini mifuko0 inazidisha matumizi kinyume na taratibu.
Alitanabahisha kuwa fao la kukosa au kupoteza ajira litatolewa kwa miezi sita ikiwa asilimia 33 ya mshahara wa mwisho wa muathirika na hivyo kupunguza makali ya maisha.
Mwongozo huo uko bayana kwa wale wanaovunja taratibu kwa kutoa adhabu au mwongozo kimaandishi namna ya kurekebisha kasoro au kuonesha nia ya kuiadhibu Bodi ya Wadhamini ya Skimu na Utawala na kutoa mapendekezo kwa mamlaka za uteuzi kwa hatua au kuchukua hatua yoyote inayoonekana kuntu kwa hali yenyewe.