31.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

SPIKA AGONGELEA MSUMARI CUF YA MAALIM SEIF

Spika wa Bunge, Job Ndugai, amegongelea msumari wa moto ndani ya Chama cha Wananchi (CUF), baada ya kukiri kupokea barua ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Shariff Hamad lakini anasita kuifanyia kazi kutokana na taarifa mkanganyiko alizopokea awali.

Katika taarifa yake aliyoitoa leo Agosti 4, Spika Ndugai amekiri kupokea barua ya Maalim Seif ya kuwafuta uanachama wabunge wawili Magdalena Sakaya ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho na Maftaha Nachuma.

“Hata hivyo, Ofisi ya Spika inayo barua ya Mwenyekiti wa chama cha CUF, Profesa Ibrahim Lipumba yenye kumbukumbu Na. CUF/AK/DSM/MKT/05/2017 ya Machi 22, mwaka huu ikiliarifu bunge kuwa Maalim Seif ameshindwa kutekeleza majukumu yake kama Katibu Mkuu kwa mujibu wa katiba ya CUF, majukumu ya Katibu Mkuu yatatekelezwa kuanzia tarehe hiyo na Magdalena Sakaya.

“Barua hiyo pia ilikuwa na kiambatanisho cha ridhaa ya mabadiliko hayo kwa barua ya Msajili wa Vyama vya siasa na Ofisi ya Spika haijawahi kupokea barua yoyote ikielezea vinginevyo, Ofisi ya Spika imenakiliwa katika barua ya msajili kwenda kwa Maalim Seif akisisitiza kutokuwapo mabadiliko mengine,” amesema Spika katika taarifa yake hiyo.

Hivi karibuni, Profesa Lipumba alimwandikia barua Spika Ndugai akimtaarifu kufutwa uanachama kwa wabunge wanane wa viti maalumu wa cham ahicho ambapo Spika alimtaarifu Msajili wa Vyama vya siasa ambaye aliwatangaza wabunge wengine wanane kujaza nafasi hizo.

Pamoja na hatua hiyo, wabunge hao waliovuliwa uanachama walifungua kesi wakitaka mahakama itoe zuio kwa bunge kuwaapisha wabunge hao wapya hadi pale itakapoamriwa. Hata hivyo, leo Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia mbali maombi hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles