25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

USAIN BOLT AMTAJA MRITHI WAKE

LONDON, ENGLAND

BINGWA wa riadha duniani katika mbio fupi, Usain Bolt, amemtaja Wayde van Niekerk kuwa mrithi wake kwenye mchezo huo mara baada ya kustaafu.

Bolt, mwenye umri wa miaka 30, ametangaza kuwa baada ya kumalizika kwa michuano ya dunia ya riadha ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi leo hii mjini London, atastaafu mchezo huo.

Amedai kuwa, mwanariadha huyo, ambaye anafanya vizuri na anakuja kwa kasi, ni Niekerk, raia wa nchini Afrika Kusini, hivyo anaamini anaweza kuja kuchukua nafasi yake ya ubora duniani.

“Van Nieker kwa kweli ameonyesha kuwa yeye ni nyota wa dunia, siwezi kumfananisha na mtu mwingine kwa kipindi hiki, ninaamini nikifanya maamuzi ya kustaafu yeye atakuwa ni mtu sahihi wa kuchukua nafasi yangu, sina wasiwasi na mwanariadha huyo,” alisema Bolt.

Bolt amekuwa kivutio kikubwa cha riadha duniani, baada ya kushinda mbio za mita 100 na 200 mjini Beijing mwaka 2008.

Niekerk, mwenye umri wa miaka 25, alishinda dhahabu katika mbio za mita 400 kwenye mashindano ya olimpiki mwaka jana nchini Brazil, huku akitumia sekunde 43.03.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles