30 C
Dar es Salaam
Saturday, December 4, 2021

LAMPARD AJIUNGA NA BT SPORT

LONDON, ENGLAND

NYOTA wa zamani wa soka wa klabu ya Chelsea, Frank Lampard, amejiunga na BT Sports kwa ajili ya kufanya uchambuzi wa michezo na anatarajia kuanza kazi rasmi Jumapili hii kwenye mchezo wa Ngao ya Hisani kati ya Arsenal dhidi ya Chelsea, katika Uwanja wa Wembley, jijini London.

Mbali na mchezaji huyo, nyota huyo ataendelea kufanya hivyo kwenye michuano mbalimbali, ikiwa pamoja na Ligi Kuu nchini England, Kombe la FA, Ligi ya Mabingwa Ulaya na michuano ya Kombe la Europa.

“Ninajisikia kuwa na furaha kubwa kujiunga na kituo hiki cha uchambuzi cha BT Sport, tutakuwa Mubashara kwenye Uwanja wa Wembley, Jumapili hii katika mchezo wa Ngao ya Hisani kati ya Arsenal na Chelsea,” alisema Lampard

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 39, baada ya kumalizana na klabu ya New York City mwaka jana, alifanikiwa kujiunga na kituo cha Sky Sports kwa mkataba wa mwaka mmoja.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,968FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles