29.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

SINGIDA UNITED YAZIDI KUNEEMEKA

Na MOHAMED KASSARA

-DAR ES SALAAM

TIMU ya Singida United imezidi kuneemeka, baada ya kuingia mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya zaidi ya Sh mil. 250 na kampuni ya usambazaji mbolea ya YARA Tanzania.

Huo ni udhamini wa tatu kwa klabu hiyo, baada ya awali kuingia mikataba na kampuni za SportPesa na Benki ya NMB.

Akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba huo, Mkurugenzi wa Yara, Alexandre Maledo, alisema kitendo cha klabu ya Singida United kutumia nembo ya zao la alizeti kimewavutia na kuona umuhimu wa kufanya nayo kazi kutokana na kampuni yake kujihusisha na kilimo.

“Mbali na kujihusisha na kilimo, mimi binafsi napenda mpira, hivyo nikaona si vibaya tukafanya nao kazi kwa pamoja, kwa kuwa hata wao wapo kwenye kampeni ya kutangaza kilimo na ufugaji Tanzania, jambo tunalolipa kipaumbele,” alisema.

Kwa upande wake, Meneja wa Singida United, Festo Sanga, alisema udhamini walioupata utazidi kuwafungulia njia ya kupata wadhamini wengi na kuifanya timu yake kushiriki ligi kwa ufanisi mkubwa.

“Singida United tumepanga timu yetu isiwe na njaa kama zinavyokuwa nyingine, ndiyo maana tunahangaika kuhakikisha tunapata wadhamini zaidi ili tuweze kushindana kikamilifu,” alisema.

Naye Kocha wa Singida United, Hans van der Pluijm, alisema udhamini huo ni chachu ya timu yake kufanya vizuri msimu ujao.

“Nina furaha baada ya mafanikio yangu Yanga, sasa napata fursa nyingine nzuri ya kuendeleza mafanikio hayo Singida United, na kwa udhamini huu tunaoupata, ni wazi kikosi changu kitafanya vizuri msimu ujao,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles