31.2 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Simba yakwepa hujuma Mbeya

Simba-vs-Yanga-2NA PENDO FUNDISHA, MBEYA

TIMU ya soka ya Simba imebuni mbinu mpya ya kufanya mazoezi ndani ya Uwanja wa Jeshi wa JKT mkoani Mbeya, ili kukwepa vitendo vya hujuma wanavyoweza kufanyiwa kwa kuruhusu mashabiki kuingia kienyeji na kuwasoma wakati wakijiandaa na mchezo dhidi ya Tanzania Prisons.

Kitendo cha Simba kuingia mafichoni na kuutumia uwanja huo ambao awali waliugomea kabla ya kucheza na Mbeya City, kimetafsiriwa kama moja ya mipango na mikakati ya timu hiyo iliyoandaliwa ili kuimarisha ulinzi kwa kuwahofia wapinzani wao.

Kabla ya kuhamia katika uwanja wa jeshi, Kocha Mkuu wa Simba Mwingereza, Dylan Kerr, alianza kuwapa wachezaji wake mbinu za kuivaa Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine kukiwa na jua kali ili kuhakikisha malengo yake ya kuondoka na pointi sita kwenye uwanja huo yanatimia.

Mashabiki wa Simba mkoani Mbeya wameanza kunogewa na mikakati ya ushindi inayowekwa na kocha huyo huku akitaka kuvunja rekodi ya makocha waliowahi kuinoa Simba na kushindwa kutamba katika Uwanja wa Sokoine na kuwafikia watani wao wa jadi, Yanga.

Katika mchezo uliopita Simba waliwachanganya Mbeya City na kuwavuruga kisaikolojia kwa kuhakikisha wanafanya mazoezi mfululizo katika uwanja huo ambapo waliweza kuibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 lakini sasa wamewakomesha maafande wa Prisons baada kuweka ulinzi mkali.

Viongozi wa Simba walioambatana na timu wamehakikisha wachezaji wanadhibitiwa vilivyo kuelekea mchezo wa kesho kwa lengo la kutaka kuendeleza mikakati yao ya ushindi.

Kwa mara ya kwanza Jumamosi iliyopita Simba ilivunja rekodi ya kutoshinda Uwanja wa Sokoine baada ya kufanikiwa kuichapa Mbeya City bao 1-0 baada ya kushindwa kufanya hivyo misimu miwili iliyopita.

Simba waliojichimbia Mbeya wiki moja iliyopita, wameweka kambi katika Hoteli ya J Safari iliyopo maeneo ya Iyunga wakisubiri kuvaana na Prisons.

- Advertisement -
Previous article
Next article

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles