30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Siku saba mshikemshike uandikishaji wapiga kura

Na FARAJA MASINDE-DAR ES SALAAM

WAKATI vyama vya siasa vikiendelea na maandalizi ya kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji unaotarajiwa kufanyika Novemba 24, mwaka huu, sasa ni wazi mshikemshike inahamia katika vituo vya uandikishaji wapiga kura.

Hatua hiyo ya uandikishaji ambayo itafanyika mwezi ujao ikienda sambamba na mchakato ndani ya vyama vya siasa kuteua wagombea wa nafasi za uenyekiti wa mtaa na wajumbe wake.

Kwa mujibu wa kanuni ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa ya mwaka 2019, kifungu 11(3)  kinaelekeza utaratibu wa uandikishaji wapigakura katika vituo.

Kwa mujibu wa kifugu hicho kinaeleza kuwa “Chama cha Siasa kitaruhusiwa kuteua wakala wake kwa kila kituo cha uandikishaji wa wapiga kura wakati wa uandikishajiwa wapiga kura,” inaeleza kanuni hiyo

Pamoja na hali hiyo pia kifungu 11(1) imefafanua utaratibu wa uandikishaji ambapo inasema kuwa, uandikishaji na uandaaji wa orodha ya wapiga kura utaanza siku ya 47 kabla ya siku ya uchaguzi na utafanyika kwa muda wa siku saba kwa kutumia fomu iliyoanishwa ambapo vituo vitakuwa kwenye majengo ya umma na pale ambapo hakuna jengo la umma, uandikishwaji utafanyika kwenye sehemu ambayo msimamizi masaidizi wa uchaguzi atakuwa amekubaliana na viongozi wa vyama vya siasa.

Hata hivyo wakati wa uandikishaji wapiga kura vituo …

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles