33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Shujaa wa ‘Hotel Rwanda’ kukabiliwa na miaka 25 jela

 KIGALI, RWANDA

SHUJAA wa “Hotel Rwanda”, Paul Rusesabagina huenda akakubiliwa na kifungo cha miaka 25 jela iwapo atakutwa na tuhuma zinazomkabili.

Rusesabagina aliyecheza kama shujaa katika filamu ya Hollywood kuhusiana na mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994 huenda akakabiliwa na kifungo cha miaka 25 jela iwapo atapatikana na makosa kadhaa yanayomkabili, hii ikiwa ni kulingana na upande wa mshitaka.

Rusesabagina, ambaye aliwahi kutoa mwito wa mapambano ya silaha dhidi ya serikali kupitia ukurasa wa YouTube alifunguliwa mashitaka katika mahakama ya mjini Kigali Jumatatu Septemba 14, 2020 dhidi ya madai 13 ambayo ni pamoja na ugaidi na kuunda ama kujiunga na makundi mbalimbali yaliyokuwa yamejihami kwa silaha.

Msemaji wa mamlaka ya mashitaka ya Rwanda, Faustin Nkusi aliliambia shirika la habari la Reauters kwa njia ya simu kwamba kwa baadhi ya makosa ya uhalifu anaweza kukabiliwa na kifungo cha miaka 25 jela na baadhi ya makosa yanaweza kuwa na adhabu kubwa zaidi ya hadi kifungo cha maisha jela.

Kesi yake imeibua ukosoaji dhidi ya serikali ya Rais Paul Kagame ambayo inashutumiwa vikali na makundi ya haki za binadamu kwa ukandamizaji unaofanywa kwa wapinzani.

Upande wa mashitaka ulisema hukumu ya Rusesabagina itakuwa ni ya haki.

Upande wa mashitaka unapinga shutuma dhidi ya serikali kuhusiana na ukanzamizaji.

Nkusi anapingana na ukosoaji huo akisema upande wa mshitaka utahakikisha hukumu yake inakuwa ya haki.

Alinukuliwa akisema “Hii ni kesi ya kisiasa huwezi kusaka uhuru wako wa kujieleza na haki za kisiasa kwa kuwauwa watu, kuwaibia mali zao na kuwateka.”

Familia ya Rusesabagina imetoa mwito kwa mchakato huo wa kusikiliza kesi kuwa wa kimataifa huku wakiituhumu serikali kwa kumyima uwakilishi wa kisheria anaoutaka.

Nkusi na Rusesabagina walichagua mawakili wawili waliomuwakilisha mahakamani siku ya Jumatatu na kuongeza kwamba aliruhusiwa kuzungumza na mkewe na watoto wanaoishi Marekani.

Wakati familia hiyo ikiituhumu Serikali ya Rwanda kwa kumteka Rusesabagina akiwa Dubai, Nkusi alinukuliwa akisema “Alikamatwa katika ardhi ya Rwanda, katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kigali. Hiyo ndio taarifa pekee ninayoweza kuitoa. Sijui ni kwa namna gani alikuja, lakini aligundulika akiwa kwenye eneo la Rwanda na kukamatwa.”

Filamu ya “Hotel Rwanda” iliyowahi kutajwa kwenye tuzo za filamu za Oscar ilimuelezea Rusesabagina wakati huo akiwa meneja wa hoteli akitumia uhusiano wake na wasomi wa kabila ya Wahutu kuwalinda Watutsi waliokuwa walijificha wakihofia kuchinjwa na Wahutu.

Jumatatu, Rusesabagina alifikishwa mbele ya hakimu wa mahakama ya mwanzo ya Wilaya ya Kicukiro mjini Kigali kujitetea dhidi ya kusikilizwa kesi yake akiwa nje au akiwa rumande.

Lakini baada ya kufikishwa kizimbani kutwa nzima ilikuwa kuhusu ikiwa mahakama hiyo ina mamlaka kwa mujibu wa sheria kusikiliza kesi yake au la.

Mawakili wake walionyesha vipingamizi vya aina tatu huku wakishikilia kwamba mahakama hii haina mamlaka ya kuendesha kesi yake.Mawakili wake pia walisema kwamba kesi yake ilipaswa kusikilizwa katika wilaya jirani ya Gasabo kwa sababu ndipo mtuhumiwa ana makazi.

Jambo jingine mawakili walisema kwamba mashtaka yanayomkabili aliyatenda akiwa nchini Ubelgiji na kwamba kwa kiasi kikubwa ilikuwa ni mikutano ya hadhara ambayo aliifanya na kwamba alikuwa na uhuru na haki ya kuifanya mikutano hiyo.

Kuhusu uraia wa mshukiwa upande wa mashtaka umesema kwamba, Paul Rusesabagina hakuwahi kupoteza uraia wa Rwanda kwa mujibu wa sheria na kwamba kisheria anachukuliwa kama raia wa Rwanda licha ya kuwa na uraia wa nchi nyingine.

 RTRE

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles